Proverbs 5:21-23


21 aKwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana,
naye huyapima mapito yake yote.

22 bMatendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe;
kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.

23 cAtakufa kwa kukosa nidhamu,
akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.
Copyright information for SwhKC